Mshambuliaji
Luis Suarez amesema hana mpango wa kuondoka Liverpool licha ya kutakiwa
na vigogo wa La Liga, Real Madrid na Barcelona
MSHAMBULIAJI Luis Suarez amesema anapenda maisha ndani ya Liverpool na hafikirii kuondoka Anfield.Nyota
huyo wa Uruguay amemaliza msimu vizuri akiwa na Wekundu hao wa Anfield
kwa kufunga mabao 31 na kutwaa tuzo za Mwanasoka Bora wa Chama cha
Wachezaji wa Kulipwa (PFA) na ya Waandishi wa Habari za Soka.Mafanikio
hayo yanakuja baada ya kupitia msimu mgumu uliopita akifungiwa kwa
kumng'ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic - akilazimisha kupita.
Sasa
wakati tetesi za usajili zimeanza tena, Suarez, ambaye mapema wiki hii
alikanusha kuwa na nia ya kuhamia klabu nyingine kubwa Ulaya, ameamua
kuuheshimu mkataba aliosaini Desemba mwaka jana.
Furaha: Suarez alisaini mkataba mpya mapema msimu uliopita na amesema ana furaha kuwepo Liverpool
Tuzo: Nyota huyo wa Uruguay alishinda tuzo ya mwaka ya PFA, huku Eden Hazard akishinda tuzo ya mchezaji bora kijana wa mwaka.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye ameripotiwa kutakiwa na Real Madrid,
ameiambia Sky Sports kwamba: "Nilisaini mkataba kwa sababu napapenda
haps na nina furaha dana hapa. Ikiwa haunt furaha hapa huwezi kusaini
mkataba wowote,".
"Liverpool
kwangu ni moja ya timu bora duniani, kwa sababu hakuna mtu haps katika
chumba cha kubadilishia nguo anafikiri mimi no bora zaidi ya wengine na
watu hapa ndani ya Melwood wanafanya kazi vizuri,"alisema.
Chapisha Maoni