Kamishna wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, aliyeshutumu mauaji ya mwanamke wa Pakistan.
Kamishna wa Umoja wa Mataifa
anayesimamia Haki za Kibinadamu, Navi Pillay, amejiunga na maelfu ya
watu duniani wanaoshutumu vikali mauaji ya mwanamke Mpakistani
aliyepigwa mawe hadi kufa nje ya mahakama na wanachama wa familia yake
kwa madai ya kuolewa na mwanamume aliyempenda.
Mume wa mwanamke huyo - Mohammed Iqbal -
alisema kuwa alishtushwa na kukasirishwa na maafisa wa polisi
waliokuwepo karibu na mahali palipotokea kitendo hicho lakini wakakosa
kufanya lo lote kunusuru maisha yake.
"Kilichotokea ni kibaya sana. Mmoja wa jamaa
yangu alivua shati na kuwapungia maafisa wa polisi ili waweze kuingilia
lakini wakapuuza. Walishuhudia kimyakimya tu Farzana akiuawa na wao
hawakufanya lo lote," alisema Iqbal.
Mamia ya wanawake huuliwa kila mwaka nchini
Pakistan kwa kuolewa na watu wasiopendwa na familia zao, jambo ambalo
halikubaliwi katika jamii nyingi ambazo hazipendelei maisha mamboleo
yanayotambua watu kupendana kabla ya kuoana.
Makundi mbalimbali ya kupigania haki za
kibinadamu kote duniani hutoa wito kwa Serikali ya Pakistan kuhakikisha
kuwa wanaoshiriki mauaji kama haya wanashtakiwa; lakini juhudi zao
zimeambulia patupu.
Chapisha Maoni