Wanjeshi hao wamemlaumu kamanda wao kwa kusababisha mauaji ya wenzao
Wanajeshi nchini Nigeria, wamemfyatulia risasi kamanda wao mkuu katika mji wa Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa nchi.
Hata hivyo Meja Jenerali, Ahmed Mohammed
alinusurika kifo. Shambulizi lilifanywa dhidi ya gari lake katika kambi
ya jeshi ya Maimalari .
Wanajeshi hao walimlaumu kamanda kwa mauaji ya wanajeshi wenzao walioshambuliwa na kundi la Boko Haram na kuuawa.
Wakati huohuo, Rais wa Goodluck Jonathan amesema
hayuko tayari kubadilishana wasichana miambili waliotekwa nyara na
wapiganaji wa Boko Haram wanaozuiliwa katika magereza ya Nigeria.
Wazazi wa wasichana waliotekwa nyara na Boko Haram
Waziri wa serikali awali alikuwa amesema kuwa
maafisa wa utawala walikuwa tayari kwa mazungumzo na Boko Haram lakini
Rais Goodluck Jonathan amesisitiza kwamba swala hilo halitazungumziwa.
“Amesisitiza kwamba hataongea na Boko Haram
kuhusu kubadilishana wasichana waliotekwa na wapiganaji wa kundi hilo
wanaozuiliwa nchini humo,” alisema mwakilishi wa serikali ya Uingereza
Mark Simmonds baada ya kukutana na Rais Jonathan kujadili namna ya
kuwanusuru wasichana hao.
Hatua ya kutekwa nyara kwa wasichana hao katika
jimbo la Borno tarehe 14 Aprili, imesababisha kero kubwa kwa jamii ya
kimataifa kiasi cha kulazimisha baadhi ya nchi za kutoa wataalamu
kusaidia serikali ya Nigeria kuwatafuta wasichana hao
Chapisha Maoni