MADHARA YATOKANAYO NA KUANGALIA SANA TV (TELEVISION)
Watu wanaotazama runinga kwa saa tatu au zaidi kila siku wako katika hatari ya kuaga dunia mapema kuwaliko wale wanaotazama kwa muda mchache. Hii ni kwa mujibu wa uchunguzi uliochapishwa katika jarida la the American Heart Association nchini Marekani. "Utazamaji sana wa wa runinga ni tabia ya watu wasio na kazi ya kufanyatu na kuna ongezeko la mienendo ya kila aina ya tabia za kukaa tu," mtafiti mkuu Miguel Martinez-Gonzalez, profesa wa chuo kikuu cha Navarra iliyoko Pamplona, nchini Uhispania, alisema katika taarifa ya shirika hilo. "Matokeo ya utafiti wetu ni sambamba na utafiti tuliowahi kufanya, ambapo muda unaotumiwa kutazama runinga uliolinganishwa na idadi ya vifo vinavyotokea kwa sababu hiyo." Watafiti hao waliwachunguz vijana wachanga 13,284 kutoka Uhispania wenye afya na waliohitimu chuo kikuu kuhusu aina tatu ya tabia za kukaa tu na hatari ya kuaga dunia kutokana na sababu zote:muda wa kutazama runinga, muda ...