Watu
wanaotazama runinga kwa saa tatu au zaidi kila siku wako katika hatari
ya kuaga dunia mapema kuwaliko wale wanaotazama kwa muda mchache.
Hii ni kwa mujibu wa uchunguzi uliochapishwa katika jarida la the American Heart Association nchini Marekani.
"Utazamaji
sana wa wa runinga ni tabia ya watu wasio na kazi ya kufanyatu na kuna
ongezeko la mienendo ya kila aina ya tabia za kukaa tu," mtafiti mkuu
Miguel Martinez-Gonzalez, profesa wa chuo kikuu cha Navarra iliyoko
Pamplona, nchini Uhispania, alisema katika taarifa ya shirika hilo.
"Matokeo ya
utafiti wetu ni sambamba na utafiti tuliowahi kufanya, ambapo muda
unaotumiwa kutazama runinga uliolinganishwa na idadi ya vifo
vinavyotokea kwa sababu hiyo."
Watafiti hao
waliwachunguz vijana wachanga 13,284 kutoka Uhispania wenye afya na
waliohitimu chuo kikuu kuhusu aina tatu ya tabia za kukaa tu na hatari
ya kuaga dunia kutokana na sababu zote:muda wa kutazama runinga, muda wa
kutumia tarakilishi na muda wa kuendesha gari.
'Sababu nyinginezo'
Vijana hao
walioshiriki, ambao walikuwa na umri wa wastani wa miaka 37 na ambao
asilimia 67 walikuwa wanawake, walifuatiliwa kwa takriban miaka 8.2.
mwishowe, vifo 97 viliripotiwa, vikiwemo vifo 19 vilivyotokana na
mishipa na moyo, 46 kutokana na saratani na mengine 32 vilivyotokana na
sababu nyinginezo.
Utafiti huo
ulionyesha hatari kubwa ya kuaga dunia ilikuwa mara mbili zaidi kwa
washiriki walioripoti kutazama runinga kwa saa tatu au zaidi kwa siku
ikilinganishwa na wale waliotazama kwa saa moja au chini ya saa.
Watu 19 waliripotiwa kufariki kutokana na kutizama TV kwa muda mrefu
Hatari hii
mara mbili zaidi ilidhihirishwa pia baada ya kutoa hesabu ya safu kubwa
ya vigezo vingine vinavyohusiana na hatari kubwa ya kuaga dunia.
Watafiti hao
hawakupata ushirikiano kati ya muda unaotumiwa na mtu anapotumia
tarakilishi au kuendesha gari na hatari kubwa ya kuaga dunia mapema
kutokana na sababu zote.
Pia
waliongezea kuwa utafiti zaidi unapaswa kufanywa ili kudhibitisha ni
athari zipi zilizopo kati ya kutumia tarakilishi na kuendesha gari
katika viwango vya vifo, na pia kutathmini taratibu za kibayolojia
zinazoweza kueleza uhusiano huo.
"Watu
wanapoendelea kuzeeka, tabia za kukaa tu zitaenea zaidi, hasa kutazama
runinga, na hili litasababisha mzigo mkubwa katika ongezeko la matatizo
ya kiafya yanayoambatana na kuzeeka," Martinez-Gonzalez alisema.
"Matokeo ya
utafiti wetu yanapendekeza watu wazima wajihusishe katika mazoezi ya
viungo, waache kukaa tu kwa muda mrefu, na wapunguze kutazama
televisheni kwa zaidi ya saa mbili kila siku."
BBC
Chapisha Maoni