Hili kundi ni kundi la kipekee miongoni mwa makundi ya Whatsapp, kwani ni kundi ambalo limeamua liwe ni la kimaendeleo zaidi na si tu kuishia kuchati. Kwani makundi yaliyomengi ndo huwa yapo hivyo. Kundi hili la AMANI TANZANIA limejaribu kujiwekea malengo ambayo faida yake huja kupatikana kwa badae, miongoni mwa malengo hayo ni ikiwemo kusaidiana wao kwa wao katika dhiki na hata faraja mbali mbali. Mwanahabari wetu alipata nafasi ya kuzfanya mahojiano na kiongozi wa kundi hilo Bi. Maryam kuwa kundi letu lina malengo mengi sana, kwani pia tumeazimia endapo mfuko wa kundi utakapokuwa umekuwa tunaweza kumkopesha mwanakundi kiasi fulani cha pesa na kurejesha pasipokuwa na riba. Alisema Maryam. Kwa kweli hii ni hatua nzuri sana kwa vijana wa leo, ipo haja ya makundi mengine nayo yangeweza kuiga yote yanayofanywa na kundi hili kwa lengo la kujipatia maendeleo zaidi.
Baadhi ya wanakikundi cha AMANI TANZANIA wakijadili masuala ya kimaendeleo
Huyo wa kwanza kulia ni Mufandish, wapili yake ni Gabriel, watatu ni Mwanamkasi, wanne ni Maryam na wa tano ni Sada
Ndugu Mufandish akifafanua jambo hapo
Chapisha Maoni