Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2016

AJALI MBAYA YATOKEA KARIAKOO USIKU HUU.

Picha
 Basi lililogonga treni likionekana kwa ndani mara baada ya ajali hiyo kutokea Taarifa iliyotufikia hivi punde, inaeleza kuwa Basi la UDA lenye namba za usajili T 696 CVP limegonga treni katika eneo la Kamata Jijini Dar es Salaam usiku huu wakati Basi hilo likotokea stendi ya Gerezani Kariakoo kuelekea Mbagala, inadaiwa kuna watu wamejeruhiwa katika ajali hiyo huku wengine wakidhaniwa kupoteza maisha. tutawaletea taarifa kamili baada ya kuipata kutoka vyombo vya Ulinzi wa Usalama jijini Dar es  salaam.  

MWANAMKE KUONGOZA MAREKANI?

Picha
Hilary Clinton amekuwa mwanamke wa kwanza kuongoza katika kinyang'anyiro cha urais ndani ya chama kikubwa nchini Marekani. Wajumbe wa Mkutano mkuu wa chama cha Democratic nchini Marekani wamemchagua seneta wa zamani na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje kuwa mgombea Urais kupitia chama hicho. Mpinzani wake mkuu Bernie Sanders alimaliza mchakato huo wa kuwania nafasi hiyo ya kukiwakilisha chama kwa kuwataka wajumbe, kumchagua Bi Clinton kwa kauli moja.

MAJALIWA: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII NI VEMA MKAJIPANGA VIZURI

Picha
waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kujipanga vizuri na kufanya mapitio ya idara zake hususan ya misitu baada ya kubainika kuwepo kwa matatizo makubwa. "Eneo la misitu limekuwa na matatizo makubwa, watendaji wengi si waaminifu na sura ya wizara si nzuri miti mingi inakatwa na fedha haiingii Serikalini. Huu ni mgogoro mpya" alisema. Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana alipokutana na watumishi wa wizara hiyo jana (Jumatatu, Julai 18, 2018) jijini Dar es Salaam, na kusisitiza kwamba hakuna sababu ya Serikali kuendelea kuwa na watumishi wasiokuwa na uaminifu, uadilifu na uwajibikaji Na: Yussuf Mufandish