MAJALIWA: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII NI VEMA MKAJIPANGA VIZURI
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kujipanga vizuri na kufanya mapitio ya idara zake hususan ya misitu baada ya kubainika kuwepo kwa matatizo makubwa.
"Eneo la misitu limekuwa na matatizo makubwa, watendaji wengi si waaminifu na sura ya wizara si nzuri miti mingi inakatwa na fedha haiingii Serikalini. Huu ni mgogoro mpya" alisema.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana alipokutana na watumishi wa wizara hiyo jana (Jumatatu, Julai 18, 2018) jijini Dar es Salaam, na kusisitiza kwamba hakuna sababu ya Serikali kuendelea kuwa na watumishi wasiokuwa na uaminifu, uadilifu na uwajibikaji
Na: Yussuf Mufandish
Lebo:
habari
Chapisha Maoni