Hilary Clinton amekuwa mwanamke wa kwanza kuongoza katika kinyang'anyiro cha urais ndani ya chama kikubwa nchini Marekani.
Wajumbe
wa Mkutano mkuu wa chama cha Democratic nchini Marekani wamemchagua
seneta wa zamani na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje kuwa mgombea Urais
kupitia chama hicho.
Mpinzani wake mkuu Bernie Sanders alimaliza
mchakato huo wa kuwania nafasi hiyo ya kukiwakilisha chama kwa kuwataka
wajumbe, kumchagua Bi Clinton kwa kauli moja.
Chapisha Maoni