Mamlaka ya dawa na chakula nchini (TFDA) imefanya ziara yake leo
katika shule ya sekondari Kazamoyo iliyopo wilaya ya Rufiji mkoani
Pwani.
TFDA Ni mamlaka ianayofanya kaza ndani ya wizara ya afya na
hasa kuhakikisha kunapatikana udhibiti mzuri wa matumizi ya vipodozi
ili kuokoa afya za watanzania kwa ujumla. Udhibiti huu unaanzia pale
ambapo kipodozi kinatoka hadi kufika kwa mtumiaji.
TFDA
Imeweza kutoa mafunzo mbalimbali kwa wanafunzi pamoja na walimu
yanayohusu matumizi ya vipodozi. Kwani imeonekana asilimia kubwa ya
watanzania wanatumia vipodozi ambavyo vina athari kiafya. Hivyo TFDA
imeweka bayana vipodozi ambavyo ni tatizo kwa mwanadamu na vile ambavyo
si tatizo kwa mwanadamu. Vipodozi ambavyo ni tatizo kwa mwanadamu TFDA
walijaribu kuvionesha vichache ambavyo walikuwa navyo kwa muda huo na
utavikuta katika picha hapo chini, ila kwa maelezo zaidi na ufafanuzi
zaidi unaweza kuwatembelea katika ofisi zao zilizopo maeneo mbalimbali
hapa nchini, kwa wale wa Dar Es Salaam ofisi za TFDA zipo pale Mabibo
barabara ya mandela.
MATUKIO KATIKA PICHA
Wawezesha wa TFDA wakijipanga kutoa somo kwa wenyeji wao
Wanafunzi wa Shule ya sekondari Kazamoyo wakiwa makini kusikiliza somo
Mwezeshaji akiendelea kutoa somo
Walimu wa Shule ya Sekondari Kazamoyo wakiwa makini kumsikiliza mwezeshaji akitoa somo
Mwezeshaji akikielezea kipodozi cha JARIBU namna kilivyokuwa na athari katika mwili wa mwanadamu
Walimu na wanafunzi wakiwa makini kusikiliza somo
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kazamoyo ndugu George N. Muhoji akikiangalia kwa umakini kipodozi aina ya Carlolight ambacho ni hatari zaidi kwa watumiaji.
Hivi ni baadhi ya vipodozi hatarishi kwa mwanadamu ambavyo TFDA walikuwa navyo kama sampo
Mwezeshaji akionesha kipodozi hatarishi maarufu sana kwa kuongeza MAKALIO hasa kwa wanawake
TAZAMA VIPODOZI AMBAVYO VINATAMBULIWA NA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA)
Chapisha Maoni