Tanzania na Rwanda zimepiga marufuku uingizaji, usambazaji na utumiaji wa simu za Samsung aina ya Galaxy Note 7.
Hatua
hiyo imechukuliwa baada ya visa vya simu hizo kulipuka na kushika moto
kuripotiwa nchi mbalimbali, jambo lililoifanya kampuni hiyo kutangaza
haitaunda tena simu hizo.
Aidha, Samsung iliwashauri wote waliokuwa wamenunua simu hizo kuzizima na kutozitumia tena.
Nchi
hizo mbili za Afrika Mashariki zimefikia uamuzi huo katikati ya wiki
iliyopita huku nchi nyingine kama Kenya zikisema hatua ambazo kampuni ya
Samsung imezichukua hadi sasa zinatosha.
Kwa
mujibu wa gazeti la The East African, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya
Mawasiliano TanzaniaBw Innocent Mungy, amewataka wananchi wote ambao
wamenunua simu hizo kuzizima na kuzirudisha katika maduka waliyonunulia
na wauzaji hao kufuata masharti ya usalama yaliyowekwa na kampuni ya
Samsung
"Tumepiga marufuku uingizwaji na utumiaji wa simu hizo," amesema Bw Mungy.
Mashirika mengi ya ndege barani Australia, Ulaya,
Asia na Marekani yamepiga marufuku wasafiri kuwa na simu hizo wakati wa
safari.
]Simu ya Samsung Note 7 ilishika moto ikifanyiwa uchunguzi maabarani Singapore
Samsung
lilitangaza kuzitoa simu hizo sokoni mwezi Septemba baada ya taarifa
kuwa baadhi ya simu hizo zilishika moto wakati wa kuchaji. Wateja
walipewa simu nyingine lakini baadaye ilibainika kwamba hata hizo mpya
zilikuwa zinashika moto.Ni hapo ambapo kampuni hiyo iliamua kusitisha kabisa uundaji wa Galaxy Note 7.
Chapisha Maoni