"MADIWANI NA WATENDAJI WAJIBIKENI KWA NAFASI ZENU" EDWARD GOWELE MKUU WA WILAYA YA RUFIJI

 


Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele amewataka Madiwani pamoja na Watendaji kuwajibika kwa nafasi zao katika kutatua changamoto za Wananchi na kuacha kuingiza maslahi binafsi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

 Ameyasema hayo wakati akitoa maelekezo ya Serikali katika kikao cha robo ya nne cha baraza la madiwani mwaka 2020/2021 kilichofanyika septemba 16.2021 katika ukumbi wa halmashauri Wilayani humo.

“ Serikali inatoa fedha nyingi kuja kwenye maeneo yetu. Tusimamie ile miradi itekelezeke kwa ubora na ikamilikie kwa wakati. Kama utahusika kuhujumu miradi ya maendeleo uwe ni Diwani au Mtendaji, mimi nitatekeleza jukumu langu. Tuache kuishi kwa mazoea.” Alisema. 

 Kwa upande wa mapato, ameagiza kusimamia utoroshwaji wa mazao ya misitu ili kuongeza mapato ya Halmashauri huku akitoa msisitizo kwa madiwani na watendaji kutohusika na njama za utoroshwaji.

“ Kwakweli hatutafumbia macho. Mimi na timu yangu tumejipanga vizuri na tunataarifa ya nini kinafanyika sehemu zote. Sasa niwaombe tusiingie huko kama uliingia kwenye miradi na ulishafanya madudu huko nyuma sasa inatosha, tuingie kazini.” Alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri John Kayombo amesema, ameanzisha utaratibu wa kuhakikisha kila Diwani anapewa taarifa ya fedha za miradi zilizopelekwa kwenye kata yake na kusisitiza kuwa kazi yao itakuwa ni kusimamia na sio kuwa wajenzi ama kupeleka vifaa vya ujenzi.

“ Hoja yangu kwenu nyinyi muwe wasimamizi na msiwe wajenzi kupeleka kokoto. Mimi huwa sina mchezo kwenye kazi, tufate taratibu, kama Mwenyekiti wa maendeleo ya kata unawajibu wa kuhoji kwenye kikao na sio kuelekeza mahali pa kununua thaluji.” Alisema.

Awali, akihutubia Baraza hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Juma ligomba ametoa shukrani na pongezi kwa Baraza hilo kuhitimisha mwaka wa fedha 2020/2021 Halmashauri ikiwa na hati safi, na kuwataka Watumishi kuongeza juhudi na maarifa kuwahudumia Wananchi huku akisistiza kutomvumilia mtumishi yeyote atakayetaka kukwamisha juhudi za Serikali.

Habari picha.






Share this post :

Chapisha Maoni


Get This:Techkgp

PAGE VIEWERS

About Me

Blog Archive

Blog za rafiki zangu

Get This:Techkgp
3D Live Statistics
 
Support : The Bantu | Mufandish | Mufandish Inc
Copyright © 2011. MUFANDISH NEWS - All Rights Reserved
Template Created by Mufandish Inc Published by Mufandish Mufandish
Proudly powered by Blogger