Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele amefungua mashindano ya Mpira wa Miguu yanayojulikana kwa Jina la Mchengerwa Cup ambayo yameletwa na Mheshimiwa Mbunge wa Rufiji Ndugu Mohammed Omar Mchengerwa huku akiitaka Jamii kuunga Mkono Mashindano hayo yanayolenga kuleta hamasa, umoja, Afya na kuinua vipaji mbalimbali.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mheshimiwa Gowele amempongeza na kumshukuru Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mheshimiwa Mohammed Mchengerwa kwa namna anavyowapenda vijana.
Sanjari na ufunguzi, amekabidhi jezi kwa viongozi wa timu zote za Tarafa ya Ikwiriri.
Tukio hilo limehudhuriwa na Madiwani wa Kata zote pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na serikali.
Awali, akitoa taarifa fupi, Katibu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi Bwana Mkoba amesema zaidi ya timu 67 zinatarajiwa kushiriki mashindano hayo, na yameanza ngazi ya Tarafa, na kuongeza kuwa kila timu itapewa jezi pamoja na Mpira mmoja.
Bwana Mkoba pia alitoa ufafanuzi wa namna timu zitakavyopata zawadi, alisema kuwa washindi ambao watapata zawadi ni kuanzia mshindi wa kwanza hadi wa nne ambapo mshindi wa kwanza atajipatia shilingi milioni 1, mshindi wapili shilingi llaki 7, mshindi wa tatu laki tano, na mshindi wa nne laki tatu.
Habari Picha
Mpiga Picha: Emmanuel Kapandila
Chapisha Maoni