"TOENI ELIMU KWA WAZAZI KUHUSU UMUHIMU WA ELIMU KATIKA MAISHA" MKURUGENZI MTENDAJI RUFIJI

 


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Ndugu Jonh Lipesi Kayomb oamesikitishwa na kauli za baadhi ya wazazi za kuwataka watoto wao wajifelishe katika masomo yao ili wasiendelee na elimu.

 "Nimesononeka Sana kusikia Mzazi anamwambia mtoto nenda kafeli. Hatua hiyo sio nzuri kwenye jamii zetu. Tushuke kwenye jamii tuelimishe Wazazi na Walezi. " Alisema.

Maneno hayo aliyasema akiwa anahutubia katika kikao maalum cha wadau wa Elimu wilayani hapo kikao ambacho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Septemba 16, 2021. 

Ndugu Kayombo aliyasema hayo baada ya kuwasikia baadhi ya wazazi wakizungumzia suala la kuwataka watoto wao wajifelishe, ni jambo ambalo yeye kama kiongozi halikumpendeza hivyo akasisitiza elimu iendelee kutolewa kwa wazazi kuhusu umuhimu wa elimu katika maisha yao.

Share this post :

Chapisha Maoni


Get This:Techkgp

PAGE VIEWERS

About Me

Blog Archive

Blog za rafiki zangu

Get This:Techkgp
3D Live Statistics
 
Support : The Bantu | Mufandish | Mufandish Inc
Copyright © 2011. MUFANDISH NEWS - All Rights Reserved
Template Created by Mufandish Inc Published by Mufandish Mufandish
Proudly powered by Blogger