MKURUGENZI MTENDAJI WILAYA YA RUFIJI AMLIPIA MWANAFUNZI ADA YA ELIMU YA KIDATO CHA TANO NA SITA


Kwa kutambua umuhimu na thmani ya Elimu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji John Kayombo, amlipia ada yote ya kidato cha tano na sita Mwanafunzi wa kike aliyeongoza kwa ufaulu kidato cha nne Rufiji Mwamvita Mkangama na kuwataka wazazi kuacha kuzuia watoto kufaulu kwa kuhofia kushindwa gharama za masomo.

Akitoa shukrani mama wa binti huyo amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji  kumpatia mtoto wake vifaa vya shule pamoja na ada yote moaka kidato cha sita kwani hatua hiyo imewatia moyo wa kuendelea kumsimamia zaidi na kupunguza ukali wa maisha aliokuwa nao.

Mwamvita Mkangama, amesema msaada huo umemtia moyo wa kupambana zaidi kujikwamua na hali ngumu ya maisha iliyopo nyumbani kwao.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FAIDA ZA KIAFYA ZA KITUNGUU MAJI KATIKA MWILI WA MWANADAMU

UFAHAMU MMEA WA MLONGE NA NAMNA UNAVYOFANYA KAZI NDANI YA MWILI WA MWANADAMU