"WAZAZI AMBAO WATOTO WAO WANAZURURA HOVYO MITAANI HAWAENDI SHULENI WAKAMATWE" MH. MEJA EDWARD GOWELE


Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele ameagiza kukamatwa kwa Vijana na Wazazi wote wenye watoto ambao wana umri wa kwenda shuleni watakaonekana wanafanya biashara maeneo ya stendi na maeneo mengine muda wa masomo .

Ameyasema hayo katika kikao cha Wadau wa Elimu kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri Wilayani Rufiji.

Sanjari na hilo, amewaonya Wazazi wanaomaliza kesi za mimba kwa watoto wa shule bila kwenda mahakamani na kuwageuza mabinti hao sehemu ya kujipoatia kipato.

Pia ameitaka Jamii kukemea swala la wazazi kuwaacha Watoto wanaosoma kulea familia Jambo linalozorotesha maendeleo yao kielimu.

Gowele ameendelea kuhamasisha Jamii na Wadau mbalimbali wa Elimu kuendelea kuunga Mkono Serikali ya awamu ya sita  katika uboreshaji wa miundombinu ya Elimu kwa Shule za  Msingi na Sekondari  huku akishukuru Bank ya NMB, CAMFED  pamoja na mdau kutoka Korea kwa misaada wanayotoa katika kuboresha Elimu Wilayani humo.

Sambamba na hayo, amemshukuru  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi za miradi ya Maendeleo hususani katika Elimu kwa Wilaya ya Rufiji na kutoa pongezi kwa Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye mara kwa mara amekuwa akijitoa na kuelekeza nguvu zaidi katika uboreshaji wa huduma za Jamii hususani Elimu kwa kutoa mifuko ya sementi zaidi ya 1000 katika maeneo yenye shule shikizi kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa.

Habari Picha






Share this post :

Chapisha Maoni


Get This:Techkgp

PAGE VIEWERS

About Me

Blog Archive

Blog za rafiki zangu

Get This:Techkgp
3D Live Statistics
 
Support : The Bantu | Mufandish | Mufandish Inc
Copyright © 2011. MUFANDISH NEWS - All Rights Reserved
Template Created by Mufandish Inc Published by Mufandish Mufandish
Proudly powered by Blogger