Video hii inamuonyesha mtu huyu akichanganya unga na maji kwenye sufuria kabla ya kuusonga kwa kutumia mashine badala ya mwiko uliozoeleka na wengi wakati wa kusonga ugali. Inaelezwa kwamba mashine hiyo imeandaliwa na mtu mmoja anayeishi Kakamega, Kenya ikiwa na uwezo wa kupika ugali kwa rekodi ya muda wa dakika tatu tu.
Kwa mujibu wa mtandao wa tuko Kenya, uliochapisha taarifa za uvumbuzi huu, uandaaji wa ugali unatofautiana kati ya kabila na kabila, lakini kwa ujumla ugali mzuri ulioiva vizuri unaweza kupikwa kwa kati ya dakika 8 mpaka 15 inategemea na kiwango cha ugali wenyewe; mkubwa, wa wastani ama mdogo.
Video hii imewashangaza watu wengi kwenye mitandao ya kijamii baadhi yao wakieleza kwamba, si rahisi kupika ugali ukaiva vizuri kwa dakika tatu. "Ugali hauwezi kuiva ama kuwa tayari kwa dakika tatu. Huo sio ugali. Unaweza kuusonga lakini huo utakuwa "ugali maji". Moto hautakua umeingia ndani vizuri. Haya ni ya wataalamu," alisema Ja'Rusinga
BOFYA HAPA KUTAZAMA VIDEO HIYO YA MWANAUME ANAYEPIKA UGALI KWA MASHINE
Chapisha Maoni