WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA AZINDUA MSIKITI LEO HII KATIKA TARAFA YA IKWIRIRI WILAYANI RUFIJI

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa amefanya uzinduzi wa Msikiti Mkubwa leo ulipo katika Tarafa ya Ikwiriri wilayani Rufiji. 

Mh. Majaliwa leo mapema amefikisha salamu za Mhe.Mbunge Wa Jimbo La Rufiji Mohammed Omar Mchengerwa Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Rais Menejimenti Ya Utumishi Wa Unma Na Utawala Bora pia amemuombea udhuru kutokana na majukumu aliyopewa na Mhe.Rais  ameshindwa kujumuika leo katika hafla hii ya ufunguzi wa Msikiti mjini Ikwiriri.

Lakini pia Mhe.Waziri Mkuu hakuacha kuzungumzia suala la miundombinu wilayani hapo kwani amefikisha salaam kwa Wananchi juu ya ujenzi wa barabara ya Nyamwage-Utete yenye Km 37  kwa kiwango cha lami na kusisitiza kwamba mkataba wa ujenzi huu utasainiwa Jumatatu ijayo.

Sambamba na hilo Mhe.Waziri Mkuu pia amewaeleza Wananchi wa Jimbo la Rufiji kuhusu ujenzi wa barabara ya Ikwiriri- Mkongo yenye Km 21 kwa kiwango cha lami.

Pia Mhe.Waziri Mkuu amezungumzia ujenzi wa daraja la Mbambe litakalo ghalimu Shilling Billion 15 

Mwisho Mhe.Waziri Mkuu amewapongeza Wananchi wa Jimbo la Rufiji kwa kuchagua kiongozi sahihi Mhe.Mchengrwa  Mwenye uwezo wa Kushawishi

Habari picha


















Share this post :

Chapisha Maoni


Get This:Techkgp

PAGE VIEWERS

About Me

Blog Archive

Blog za rafiki zangu

Get This:Techkgp
3D Live Statistics
 
Support : The Bantu | Mufandish | Mufandish Inc
Copyright © 2011. MUFANDISH NEWS - All Rights Reserved
Template Created by Mufandish Inc Published by Mufandish Mufandish
Proudly powered by Blogger