Machapisho

HARAMBEE STARS KWA KWELI YAAMBULIA PATUPU

Picha
Harambee Stars imeondolewa kwenye kinyang'anyiro cha kufuzu kombe la dunia 2014 Mchuano wa kufa na kupona ulishuhudiwa kati ya bingwa wa Afrika Super Eagles wa Nigeria na Harambee Stars wa Kenya katika uwanja wa kimataifa wa Moi Kasarani mjini Nairobi. Musa Ahmed aifungia Nigeria bao la kwanza na la pekee kunako dakika ya 81. Mashabiki wa Kenya Kimya! Baadhi ya mashabiki wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars waanza kuondoka uwanjani. Mashabiki wa Nigeria hawakuwa wengi uwanjani wakikisiwa kufika 300, lakini licha ya uchache wao ,hawakufa moyo.Mandishi wa BBC Odeo Sirari aliyekuwa uwanjani,alishuhudia mashabiki wachache wa Nigeria wakiisiahngilia timu yao kwa nyimbo na ngoma japo hawakuwa wanasikika kutokana na mayowe ya wakenya. Ilikuwa mechi ya mkondo wa pili kwa timu hizo mbili baada ya kwenda sare ya bao moja kwa moja walipocheza kwa mkondo wa kwanza mjini Calabar Nigeria mwezi jana. Mechi hii ni ya kundi la F ya kugombania nafasi ya kushirik...

UGANDA YAONA NJIA YA KUELEKEA BRAZIL

Picha
Timu ya Taifa ya Soka ya Uganda, leo imeilaza Liberia kwa bao moja kwa bila na kuimarisha matumaini yake ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao nchini Brazil, katika mechi kali iliyochezwa mjini Kampala. Kufuatia ushindi huo Uganda Cranes sasa imepanda hadi nafasi ya pili katika kundi J na alama 5 nyuma ya vinara wa kundi hilo Senegal ambao wanachuana na Angola. Uganda sasa imesalia na mechi mechi mbili na imepangiwa kuchuana na Angola tarehe kumi na tano mwezi huu kabla ya kupepetana na Senegal tarehe 6 Septemba mwaka huu katika uwanja wa Leopold Senghor. Uganda ni sharti ishindi mechi zake zilizosalia ili kuwa katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa fainali hizo zitakazoandaliwa nchini Brazil Januari mwakani. Katika mechi zingine za kufuzu kwa Fainali hizo, Zambia wameilaza Lesotho kwa magoli manne mwa yai nayo Botswana wakalemewe nyumbani kwao na Ethiopia kwa kufungwa magoli mawili kwa moja.

MAANDAMANO MAKUBWA KUFANYWA KENYA DHIDI YA WABUNGE

Picha
  Mashirika yasiyo ya kiserikali yamefanya maandamano mengine mjini Nairobi Kenya kupinga jaribio la wabunge kujiongeza mishahara hata baada ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kusema kuwa hakuna pesa za kutosha kuwaongeza misahara wabunge hao. Mashirika hayo yanataka wabunge kukubali mishahara waliyowekewa na tume ya kudhibiti mishahara ya wafanyakazi wa serikali. Kulingana na tume hiyo wabunge wanapaswa kupokea dola elfu sita kila mwezi lakini wanataka pesa hizo kuongezwa hadi dola elfu kumi au shilingi laki nane za Kenya. Maandamano ya leo yanakuja siku kadhaa baada ya baadhi ya wabunge kusema kuwa tayari wamepokea mishahara ya shilingi lake nane na kupelekea tume hiyo kusema kuwa yeyote atakayepokea zaidi ya laki tano atalazimishwa kulipa pesa hizo. Pia yanakuja siku tatu baada ya bunge kufutilia mbali sherehe zake za jubilee ambapo ilitarajiwa kuruhusu wananchi kujionea bunge. Mmoja wa wandaaji wa maandamano hayo Bwana Boniface Mwangi, alisema kuwa waanda...

MOURINHO PEEKS JOHN TERRY AS CHELSEA CAPTAIN

Picha
Jose Mourinho says John Terry will stay as Chelsea club captain but has refused to be drawn on whether he wants to sign Manchester United striker Wayne Rooney. Terry, 32, was captain as Chelsea won two Premier League titles in Mourinho's first spell at Stamford Bridge. But he was not always selected by interim boss Rafael Benitez during an injury-troubled 2012-13 season. Mourinho said: "John is the club captain. I'm more than happy with that and so are the fans." “ If the best for all of us is for Fernando to stay, let's help him and try to get the best out of him ” But he insisted there would be "no privilege" for his former players and would not give centre-back Terry reassurances about a regular place, saying: "With the armband? Only when he plays. If he isn't in the starting XI he won't have the armband." Mourinho, back at Stamford Bridge for a second ...

MWANAMKE AMUUNGUZA MUMEWE KWA MAJI YA MOTO

Picha
  Mwanamke mmoja anasakwa na polisi Kabete baada ya kudaiwa kumchoma mumewe kwa maji ya sima na kisha kumficha nyumbani siku tano katika kijiji cha Muthure, eneo bunge la Kabete .  Mwanamume huyo sasa anauguza majeraha hospitali Mwanaume huyo aliokolewa na majirani baada ya siku tano za kufichwa na mkewe aliyemchoma kwa maji moto kwenye kichwa na kifua katika kijiji hicho, Majirani walishangaa walipomkosa Bw Samuel Mungai, mwanamume waliyemjua kama mcheshi na aliyependa kileo chake na ndipo wakaanza kumsaka.   Chifu wa eneo hilo Peter Njoroge alisema kuwa wanakijiji walimpata Bw Mungai huku amefungiwa katika nyumba yake na majeraha mabaya, ambayo yalikuwa yameanza kunuka, yaliyosababishwa na maji moto. “Lilikuwa jambo la kusikitisha kupata mwanaume huyu amechomeka vibaya sana kwenye kifua na kichwa,” alisema Chifu Njoroge. Mwanaume huyo, Bw Mungai alihadithia yaliyomsibu kabla ya wenyeji kumpeleka katika kituo cha polisi cha Kikuyu kuandikisha ri...