Machapisho

MECHI YA KWANZA YA MUUMIZA KICHWA MOURINHO

Picha
Kocha wa Chelsea,Jose Mourinho amesema itakua vigumu kujizuia wakati atakapokaa rasmi katika benchi ya Stamford Bridge kwa pambano lao la kwanza la Ligi Kuu ya Premier dhidi ya Hull City. Mourinho aliyejunga tena na klabu hiyo kwa awamu ya pili mnamo mwezi wa Juni baada ya kuondoka mwaka September 2007. "Nitakapoingia katika uwanja wangu,kukaa katika benchi langu pamoja na watu wangu ,itabidi niwe mtulivu kidogo,"Alisema Mourinho,mwenye umri wa miaka 50. "Itanichukua dakika mbili tatu kutafakari na kabla ya kushughulikia pambano lenyewe ." Mourinho aliwasili mara ya kwanza Stamford Bridge mwaka 2004, wiki chache tu baada ya kuiongoza Porto ya Ureno kunyakua kombe la mabingwa wa Ulaya. Alishinda kombe kombe la FA na pia Ko...

MISRI KUNAENDELEA KUCHAFUKA

Picha
Maelfu ya wafuasi wa Rais wa Misri aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi wameanza maandamano mengine mjini Cairo, huku kukiwa na hofu ya kuzuka makabiliano zaidi. Maafisa wa usalama wamezingira barabara kuelekea medani ya Ramses ambapo maandamano hayo yalipangwa kufanyika. Maandamano ya sasa yanajiri siku mbili baada ya jeshi kuvunja kambi ambapo wafuasi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood walikua wamesalia kwa zaidi ya mwezi mmoja. Makabiliano yalizuka na zaidi ya watu 600 wakauawa, maelfu walijeruhiwa.Maandamano zaidi yanaendelea nje ya mji mkuu Cairo na taarifa zinasema watu wanne wameuawa kwenye makabiliano eneo la Ismailia. Polisi wa Misri wameamrishwa kutumia risasi za moto kulijinda na kulinda majengo ya serikali dhidi ya kushambuliwa. Huku utawala wa mpito ukitangaza hali ya hatari, mwandishi wa BBC aliy...

KARIBU PISAB GENERAL COMPANYY LIMITED KWA MAENDELEO YA MAISHA YAKO. (WELCOME AT PGCL FOR YOUR BENEFIT)

PGCL IT DEALS WITH THE FOLLOWINGS: LUBRICANTS AGENTS OF ALL SPARE OF MOTOR VEHICLE IMPORTERS & EXPORTERS MILLING ENVIRONMENT CLEANERS & GENERAL SUPLPLIES WE ARE AVAILABLE AT MANZESE - ACCESS BANK CELL: +255 712 823 838               +255 754 811 535               +255 719 556 551 E-mail: pisabgeneralcompany@gmail.com work with us you are most welcome

TAARIFA ZA UCHAGUZI MKUU MALI

Picha
Ibrahim Boubacar Keita ameibuka mshindi wa uchaguzi mkuu nchini Mali huku mpinzani wake akikubali kushindwa katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais. Soumaila Cisse,amekubali kushindwa na mpinzani wake,aliyekuwa waziri mkuu Ibrahim Boubakar Keita. Bwana Cisse aliyewahi kuhudumu kama waziri wa fedha amempongeza Keita kwa ushindi huo na kumtakia kila la kheri. Bwana Keita, mwenye umri wa miaka 68, alihudumu kama waziri mkuu kutoka mwaka 1994 hadi 2000. Mali imekumbwa na vurugu kwa kipindi cha mwaka mmoja ikiwemo mapinduzi ya kijeshi na kufuatiwa na harakati za jeshi la Ufaransa kuwaondoa wapiganaji waliokuwa wameteka eneo la Kaskazini mwa nchi. Hata hivyo hakuna matokeo rasmi yametolewa kufuatia duru ya pili ya uchaguzi iliyofanyika Jumapili. Katika duru ya kwanza bwana Cisse alipata 19% dhidi ya bwana Keita aliyepata 40% Bwana Keita anayejulikana kama (IBK) - ata...

ZAIDI YA WATU 15 MISRI WAUAWA NCHINI MISRI

Picha
Zaidi ya watu kumi na watano wameripotiwa kuuwawa wakati maafisa wa usalama nchini Misri walipoanza operesheni ya kuwatimua wafuasi wa rais aliyeng'olewa madarakani Mohammed Morsi, waliokuwa wamekita kambi mjini Cairo. Lakini vuguvugu la Undugu wa Kiislamu, Muslim Brotherhood, ambalo linaunga mkono maandamano hayo limesema idadi ya waliouwawa inazidi kumi na watano. Milipuko ya risasi ilisikika na magari ya kivita yametumika kuwatimua waandamanaji hao. Maafisa wa usalama walifyatua gesi ya kutoa machozi. Maafisa wamesema kuwa kambi ya waandamanaji hao katika Medani ya Nahda magharibi mwa mji wa Cairo imevunjwa na waandamanaji kutawanywa. Wizara ya mambo ya ndani imesema kuwa operesheni ya kusafisha barabara za mji huo inaendelea. Wanaharakati wanaomuunga mkono bwana Morsi walifukuzwa hadi hifadhi ya wanyama pori iliyopo karibu pamoja na chuo kikuu cha Cairo, kituo cha televisheni kinachomilikiwa na serikali Nile TV ...

LANA:MWANAMKE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO JELA BAADA YA KUMTUPA MTOTO WAKE CHOONI

Picha
Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka  5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni. Tukio hilo lilitokea Juni 14, Mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza  kugundua kuwepo kwa Mtoto katika choo cha shimo.   Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa. Ameongeza kuwa amelazimika kutupa katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo  tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.    Rukia Haruna (31)  akitolewa nje  na Askari wa Jeshi la Polisi akitolewa nje  ya  Mahakama kwenda Gerezani kutumikia kifungo cha miaka 5 Jela     Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemtaja Mtuhumiwa kuwa ni Rukia Haruna (31) mkazi wa Manga A Jijini Mbeya na kw...

UNAYAJUA MADHARA YA UVAAJI WA SRUALI ZA KUBANA KWA WANAUME-SOMA MAKALA HII

Picha
Madaktari wamesema uvaaji wa suruali za kubana kwa wanaume ni chanzo cha baadhi kuwa wagumba na wengine kupata magonjwa ya ngozi Kampala. Kwa wananchi wa Uganda, jina la Denzel Mwiyeretsi siyo geni kwa kuwa ni mtangazaji wa masuala ya mjini katika Kituo cha Televisheni cha XFM, lakini Denzel pia ni maarufu kwa wafuatiliaji wa Big Brother kutokana na kushiriki shindano hilo nchini Afrika Kusini. Hata hivyo, watu wengi wanamfahamu kwa mitindo ya uvaaji wake wa suruali za kubana. “Mitindo ni kama umri, haiwezi kuwa vilevile. Ni kama vile mvinyo mtamu, pamoja na umri, mtindo wako lazima uwe na mwonekano mzuri. Ni kujaribu kitu kipya. Mimi ni mtu mwenye kuthubutu na napenda kujaribu vitu vipya (ikiwamo mitindo) ili kufanya maisha yangu yawe yenye mvuto,” alisema Denzel. Pamoja na tabia yake ya kupenda kuvaa suruali za kubana kuna watu akiwamo dada yake hakupendezwa na hali...