Machapisho

WATU SABA 7 WAHUKUMIWA KIFO KWA UBAKAJI

Picha
Kiongozi wa genge la washukiwa wa ubakaji nchini Afghanistan Watu saba wamehukumiwa kifo baada ya kuwabaka kwa zamu wanawake wanne nje ya mji mkuu wa Afghanista,kabul mwezi uliopita. Hukumu hiyo inajiri baada ya kesi iliochukuwa masaa mawili na nusu ambapo wawili kati ya saba hao walikana madai hayo. Mwathiriwa mmoja ilibidi alazwe hospitalini kufuatia kitendo hicho huku mwengine akidaiwa kuwa mja mzito. Hukumu hiyo ya kifo ilitolewa kwa kosa la wizi wa mabavu huku hukumu ya miaka kumi na tano ikisimamia ubakaji. Rais Hamid Karzai aliunga mkono wito wa watu hao kunyongwa hadharani iwapo watapatikana na makosa.

TAZAMA PICHA ZA KAMATI ZA BUNGE LA KATIBA MJINI DODOMA LEO.

Picha
 PICHA ZA KAMATI ZA BUNGE LA KATIBA MJINI DODOMA LEO.  Makamu Mwenyekiti wa Kamati Namba 11 ya Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Hamad Yussuf Massauni akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo kwenye ukumbi wa mikutano wa St. Gasper kuhusu mambo yaliyojiri katika Kamati yake.Kulia ni Katibu wa Kamati hiyo Bakari Kishoma.  Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakijadiliana jambo mara baada ya mapumziko ya kikao cha leo mjini Dodoma leo kwenye ukumbi wa mikutano wa St. Gasper kulia hapo ni Profesa Hamza Njozi Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro.  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Adam Malima akijadiliana jambo na mjumbe wenzake  John Cheyo mara baada ya mapumziko ya kikao cha leo mjini Dodoma leo kwenye ukumbi wa mikutano wa St. Gasper.  Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakijadiliana jambo mara baada ya mapumziko ya kikao cha leo mjini Dodoma leo kwenye ukumbi wa mikutano wa S...

KWA KWELI MICHEPUKO NI NOUMA

Picha
Akiwa katika machela hospitalini

MADHARA YATOKANAYO NA KUANGALIA SANA TV (TELEVISION)

Picha
  Watu wanaotazama runinga kwa saa tatu au zaidi kila siku wako katika hatari ya kuaga dunia mapema kuwaliko wale wanaotazama kwa muda mchache. Hii ni kwa mujibu wa uchunguzi uliochapishwa katika jarida la the American Heart Association nchini Marekani.   "Utazamaji sana wa wa runinga ni tabia ya watu wasio na kazi ya kufanyatu na kuna ongezeko la mienendo ya kila aina ya tabia za kukaa tu," mtafiti mkuu Miguel Martinez-Gonzalez, profesa wa chuo kikuu cha Navarra iliyoko Pamplona, nchini Uhispania, alisema katika taarifa ya shirika hilo. "Matokeo ya utafiti wetu ni sambamba na utafiti tuliowahi kufanya, ambapo muda unaotumiwa kutazama runinga uliolinganishwa na idadi ya vifo vinavyotokea kwa sababu hiyo."   Watafiti hao waliwachunguz vijana wachanga 13,284 kutoka Uhispania wenye afya na waliohitimu chuo kikuu kuhusu aina tatu ya tabia za kukaa tu na hatari ya kuaga dunia kutokana na sababu zote:muda wa kutazama runinga, muda ...

AJALI MBAYA YATOKEA MAFINGA

Picha
baada ya ajali hiyo,  Inavyoonekana kwa nyuma hii ni sehemu ya mbele ya gari hilo Scania lililogongwa kwa nyuma Sehemu ambayo gari hilo dogo liliingia AJALI mbaya iliyohusisha gari dogo aina ya Land Rover Freelander lenye namba T368 CVK na roli la mizigo aina ya Scania lenye namba T346 BRF imetokea usiku wa juzi katika eneo la Lugemba, kilomita kadhaa kabla ya kufika mji wa Mafinga. Taarifa za awali zinaonesha kwamba dereva wa gari hilo jina lake bado halijapatikana alifariki papohapo baada ya gari yake kuingia mvunguni mwa roli hilo lililokuwa limepaki kandokando ya barabara ya Mafinga Mkoani Iringa, akiwa katika mwendo mkali. Mwanafunzi wa kike wa Chuo Kikuu cha Tumaini aliyekuwemo katika gari hilo amenusurika kufa; binti huyo ambaye pia jina lake halikupatikana amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi baada ya kujeruhiwa vibaya ikiwa ni pamoja na kukatika mkono. Mashu...

ONA AJALI MNBAYA ILIYOTOKEA LEO MAKONGO DAR ES SALAAM

Picha
Watu kadhaa wameripotiwa kufariki Dunia kwenye ajali mbaya iliyohusisha magari matatu ikiwemo lori la mchanga huku mawili yakiwa ni ya abiria maarufu kama daladala  yanayofanya safari zake kati ya ubungo na Tegeta.   Ajali hiyo imetokea mchana kwenye eneo la kikosi cha jeshi cha Lugalo jijini Dar es salaam. Jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo mbaya iliyosababisha vifo vya watu 6, watatu wakiwa ni wanaume na watatu wakiwa ni wanawake huku hali za majeruhi ambao walikimbizwa hospitali ya Lugalo zikielezwa kuwa ni mbaya. Bado jeshi la Polisi limeendelea na uchunguzi kujua iwapo dereva wa daladala hiyo lenye nambari za usajili T 377 BEF aliyesababisha ajali hiyo kama alifanya uzembe ama la. ONA PICHA ZAIDI

JUMUIYA YA WNARUFIJI WA MUSLIM UNIVERSITY OF MOROGORO WAKAA KIKAO KIZITO KUJADILI RUFIJI YAO

Picha
Katibu mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Rufiji Pwani akizungumza katika kikao kilichofanyika juzi cha Wanajumuiya ya Watu wa Rufiji Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro hapo  Mambo Club mjini Morogoro Mheshimiwa Musa alizungumza mengi sana kuhusu Rufiji na hasa katika swala zima la sekta ya elimu, imeonekana kuwa swala la elimu Rufiji ni tatizo sana kiasi ambacho kwamba kunasababisha kuwepo kwa maendeleo duni. Mheshimimwa Musa alisisitiza sana swala la kurudi nyumbani (Rufiji) kwa lengo la kufanya kazi kwa wanarufiji ambao wanategemea kumaliza degree zao hivi karibuni baada ya mwezi mmoja. Mheshimiwa Musa alielezea kuhusu urudishwaji wa fedha za mradi wa maji amabao ungeweza kiuwasaidia warufiji kuondokana na tatizo la maji na yote haya ni kutokana kushindwa kuzitumia pesa zile kwa ajili ya mradi huo. lakini pia mheshimiwa alisema kuwa sekta nyingi Rufiji zinaongozwa na watu ambao si wazawa wa rufiji na wakati huo huo warufiji ambao ni wasomi wapo lakini wana...