Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2021

MCHENGERWA CUP YAZINDULIWA RASMI JANA KATIKA VIWANJA VYA MABATINI IKWIRIRI RUFIJI

Picha
  Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele amefungua mashindano ya Mpira wa Miguu yanayojulikana kwa Jina la Mchengerwa Cup ambayo yameletwa na Mheshimiwa Mbunge wa Rufiji Ndugu Mohammed Omar Mchengerwa huku akiitaka Jamii kuunga Mkono Mashindano hayo yanayolenga kuleta hamasa, umoja, Afya na kuinua vipaji mbalimbali. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mheshimiwa Gowele amempongeza na kumshukuru Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mheshimiwa Mohammed Mchengerwa kwa namna anavyowapenda vijana. Sanjari na ufunguzi, amekabidhi jezi kwa viongozi wa timu zote za Tarafa ya Ikwiriri. Tukio hilo limehudhuriwa na Madiwani wa Kata zote pamoja na viongozi mbalimbali wa chama na serikali. Awali, akitoa taarifa fupi, Katibu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi Bwana Mkoba amesema zaidi ya timu 67 zinatarajiwa kushiriki mashindano hayo, na yameanza ngazi ya Tarafa, na kuongeza kuwa kila timu itapewa jezi pamoja na Mpira mmoja. Bwana Mkoba pia alitoa ufafanuzi wa namna timu zitakavyopata zawadi, alis...

MKURUGENZI MTENDAJI WILAYA YA RUFIJI AMLIPIA MWANAFUNZI ADA YA ELIMU YA KIDATO CHA TANO NA SITA

Picha
Kwa kutambua umuhimu na thmani ya Elimu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji John Kayombo, amlipia ada yote ya kidato cha tano na sita Mwanafunzi wa kike aliyeongoza kwa ufaulu kidato cha nne Rufiji Mwamvita Mkangama na kuwataka wazazi kuacha kuzuia watoto kufaulu kwa kuhofia kushindwa gharama za masomo. Akitoa shukrani mama wa binti huyo amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji  kumpatia mtoto wake vifaa vya shule pamoja na ada yote moaka kidato cha sita kwani hatua hiyo imewatia moyo wa kuendelea kumsimamia zaidi na kupunguza ukali wa maisha aliokuwa nao. Mwamvita Mkangama, amesema msaada huo umemtia moyo wa kupambana zaidi kujikwamua na hali ngumu ya maisha iliyopo nyumbani kwao.

"WAZAZI AMBAO WATOTO WAO WANAZURURA HOVYO MITAANI HAWAENDI SHULENI WAKAMATWE" MH. MEJA EDWARD GOWELE

Picha
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele ameagiza kukamatwa kwa Vijana na Wazazi wote wenye watoto ambao wana umri wa kwenda shuleni watakaonekana wanafanya biashara maeneo ya stendi na maeneo mengine muda wa masomo . Ameyasema hayo katika kikao cha Wadau wa Elimu kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri Wilayani Rufiji. Sanjari na hilo, amewaonya Wazazi wanaomaliza kesi za mimba kwa watoto wa shule bila kwenda mahakamani na kuwageuza mabinti hao sehemu ya kujipoatia kipato. Pia ameitaka Jamii kukemea swala la wazazi kuwaacha Watoto wanaosoma kulea familia Jambo linalozorotesha maendeleo yao kielimu. Gowele ameendelea kuhamasisha Jamii na Wadau mbalimbali wa Elimu kuendelea kuunga Mkono Serikali ya awamu ya sita  katika uboreshaji wa miundombinu ya Elimu kwa Shule za  Msingi na Sekondari  huku akishukuru Bank ya NMB, CAMFED  pamoja na mdau kutoka Korea kwa misaada wanayotoa katika kuboresha Elimu Wilayani humo. Sambamba na hayo, amemshukuru  Rais wa Jamhur...

"TOENI ELIMU KWA WAZAZI KUHUSU UMUHIMU WA ELIMU KATIKA MAISHA" MKURUGENZI MTENDAJI RUFIJI

Picha
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Ndugu Jonh Lipesi Kayomb oamesikitishwa na kauli za baadhi ya wazazi za kuwataka watoto wao wajifelishe katika masomo yao ili wasiendelee na elimu.  "Nimesononeka Sana kusikia Mzazi anamwambia mtoto nenda kafeli. Hatua hiyo sio nzuri kwenye jamii zetu. Tushuke kwenye jamii tuelimishe Wazazi na Walezi. " Alisema. Maneno hayo aliyasema akiwa anahutubia katika kikao maalum cha wadau wa Elimu wilayani hapo kikao ambacho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Septemba 16, 2021.  Ndugu Kayombo aliyasema hayo baada ya kuwasikia baadhi ya wazazi wakizungumzia suala la kuwataka watoto wao wajifelishe, ni jambo ambalo yeye kama kiongozi halikumpendeza hivyo akasisitiza elimu iendelee kutolewa kwa wazazi kuhusu umuhimu wa elimu katika maisha yao.

"MADIWANI NA WATENDAJI WAJIBIKENI KWA NAFASI ZENU" EDWARD GOWELE MKUU WA WILAYA YA RUFIJI

Picha
  Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele amewataka Madiwani pamoja na Watendaji kuwajibika kwa nafasi zao katika kutatua changamoto za Wananchi na kuacha kuingiza maslahi binafsi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.  Ameyasema hayo wakati akitoa maelekezo ya Serikali katika kikao cha robo ya nne cha baraza la madiwani mwaka 2020/2021 kilichofanyika septemba 16.2021 katika ukumbi wa halmashauri Wilayani humo. “ Serikali inatoa fedha nyingi kuja kwenye maeneo yetu. Tusimamie ile miradi itekelezeke kwa ubora na ikamilikie kwa wakati. Kama utahusika kuhujumu miradi ya maendeleo uwe ni Diwani au Mtendaji, mimi nitatekeleza jukumu langu. Tuache kuishi kwa mazoea.” Alisema.   Kwa upande wa mapato, ameagiza kusimamia utoroshwaji wa mazao ya misitu ili kuongeza mapato ya Halmashauri huku akitoa msisitizo kwa madiwani na watendaji kutohusika na njama za utoroshwaji. “ Kwakweli hatutafumbia macho. Mimi na timu yangu tumejipanga vizuri na tunataarifa ya nini kinafanyi...

CCM YAWATAKA VIONGOZI, WATENDAJI WA CHAMA NA SERIKALI KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA WANANCHI

Picha
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi( CCM) Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amewaeleza viongozi na watendaji wote ndani ya Chama na Serikali kushughulikia changamoto za wananchi badala ya kukaa maofisini tu. Shaka ameyasema hayo  akiwa ziarani  wilayani Nachingwea Mkoani  Lindi. Pamoja na mambo mengine ziara hiyo imelenga kuhamasisha na kuimarisha uhai wa chama kuanzia ngazi ya shina, kuhimiza mahusiano ndani ya chama pamoja na serikali. Shaka ameendelea kuwahakikishia wananchi kuwa CCM na serikali vipo salama na imara katika mikono ya Mwenyekiti na Rais mahiri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. "Hii ni kwa sababu katika muda mfupi serikali anayoiongoza imetoa mwelekeo wenye matumaini makubwa ya kuimarisha ustawi wa wananchi, uchumi wa nchi yetu, kuvutia uwekezaji zaidi, kuzalisha ajira kwa vijana na kuimarisha ulinzi na usalama wa mipaka ya Nchi yetu na raia wote,"amesema Shaka Shaka amewataka viongozi na watendaji wot...