Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2021

TAZAMA FAIDA ZA MBAAZI LEO HII ILI UJUE NAMNA GANI UNAWEZA KUJITIBU KWA KUTUMIA MBAAZI

Picha
Mbaazi ni moja ya dawa za mitishamba zinazotibu mambo mengi ikiwemo kurudisha bikra ya msichana endapo majani yake yatatumika na kuandaliwa vyema. Tuwe makini katika kufuata njia za kuandaa dawa yetu. MAANDALIZI YA KUANDAA MAJANI YA MBAAZI (kwa wanawake) Chukua majani ya mbaazi kisha yatwang Weka maji kidogo vaa kama pedi kwa muda wa wiki utaona mabadiliko FAIDA ZA KUTUMIA MAJANI YA MBAAZI (kwa wanawake) Kukausha uke Kuondoa majimaji ukeni Kuongeza joto ukeni wakati wa jimai Kuongeza hamu ya tendo la ndoa Husogeza kizazi karibu Kusafisha kuta za uke NB : Mbaazi ni mti wenye maajabu makubwa kuanzia Mizizi yake mpaka majani TIBA KWA WATU WOTE Dawa hii inaweza kutibu magonjwa yafuatayo 1-Inauwezo mkubwa wa kushusha homa 2-Husaidia kuponesha vidonda. 3-Husaidia kurekebisha mzunguko wa hedhi kwa wanawake. 4-Husaidia kupunguza uvimbe 5-Huponyesha kifua na kukohoa. 6-Husafisha kibofu/njia ya mkojo. 7- Huongeza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbali mbali

WALIMU WA SHULE YA SEKONDARI UMWE WAFANYA TAFRIJA YA KUJENGA MAHUSIANO MAZURI LEO KAZINI

Picha
  Walimu wa shule ya Sekondari Umwe iliyopo Kata ya Umwe Tarafa ya Ikwiriri Wilayani Rufiji wafanya tafrija fupi ambayo inalenga kukuza mahusiano mazuri kazini. Tafrija fupi ambayo imeongozwa na Mkuu wa Shule hiyo Ndugu Bakari Elisafi Mfingi ilifanyika kwa kuchinja Mbuzi, Kuku pamoja na chakula cha pamoja. The Bantu ilifanya mahojiano na Mkuu wa Shule hiyo akisema kuwa hii ni sehemu ya utaratibu wetu kama Stuff kujumuika pamoja kwa siku moja kwa kila term tukiwa na dhamira ya kukuza uhusiano kazini kwani tunaamini kuwa mahusiano mazuri kazini ndiyo yanayoleta ufanisi katika utendaji kazi wetu. Alisema Mfingi. Habari Picha

TASSAF KUWAJENGEA WALENGWA NGURYATI KIWANDA KIDOGO

 

"VIONGOZI MSIWATUKANE NA KUWADHALILISHA WATUMISHI WA UMMA MBELE ZA WATU" MH. MCHENGERWA

 

"WAKURUGENZI NA WAKUU WA WILAYA MKAHOISHE VITENGO VYA HABARI KWENYE HALMASHAURI ZENU" MH. MCHENGERWA

 

MASHINE YA KUPIKIA UGALI KWA DAKIKA TATU (3) YAGUNDULIWA NCHINI KENYA

Picha
Video hii inamuonyesha mtu huyu akichanganya unga na maji kwenye sufuria kabla ya kuusonga kwa kutumia mashine badala ya mwiko uliozoeleka na wengi wakati wa kusonga ugali. Inaelezwa kwamba mashine hiyo imeandaliwa na mtu mmoja anayeishi Kakamega, Kenya ikiwa na uwezo wa kupika ugali kwa rekodi ya muda wa dakika tatu tu. Kwa mujibu wa mtandao wa tuko Kenya, uliochapisha taarifa za uvumbuzi huu, uandaaji wa ugali unatofautiana kati ya kabila na kabila, lakini kwa ujumla ugali mzuri ulioiva vizuri unaweza kupikwa kwa kati ya dakika 8 mpaka 15 inategemea na kiwango cha ugali wenyewe; mkubwa, wa wastani ama mdogo. Video hii imewashangaza watu wengi kwenye mitandao ya kijamii baadhi yao wakieleza kwamba, si rahisi kupika ugali ukaiva vizuri kwa dakika tatu. "Ugali hauwezi kuiva ama kuwa tayari kwa dakika tatu. Huo sio ugali. Unaweza kuusonga lakini huo utakuwa "ugali maji". Moto hautakua umeingia ndani vizuri. Haya ni ya wataalamu," alisema Ja'Rusinga BOFYA HAPA KUTA...

JOHN DUMELO AREKODI FILAMU YA 'MULASI THE DEATH' NGORONGORO NA SERENGETI, TANZANIA

Picha
  NYOTA wa Filamu na mshindi wa tuzo nyingi za uigizaji nchini Ghana John Dumelo yupo nchini Tanzania akiandaa filamu ya 'Mulasi The Death' katika maeneo mawili ya utalii ya Ngorongoro na Serengeti mtandao wa tanzaniatimes.net umeripoti. Dumelo yupo na timu inayoongozwa na mtanzania aishiye Marekani Honeymoon Aljabri ambaye pia ni mtunzi, mtayarishaji na muongozaji wa filamu aliyeshinda tuzo kadhaa nchini Marekani. Dumelo ameeleza, licha ya kuwa na shughuli kubwa ya kurekodi filamu amevutiwa zaidi mandhari na uzuri wa mbuga za wanyama pamoja na huduma bora zinazotolewa katika vivutio vya Serengeti na Ngorongoro. "Hii ni mara yangu ya pili kufika Tanzania, lakini nchi hii haishi kunishangaza, lazima nirudi kwa ziara ndefu ya utalii," amesema Dumelo ambaye ameshiriki kwenye filamu zipatazo 60 zikiwemo za A Northern Affair, Private Storm, na Tales of Nazir. John Dumelo ameshinda tuzo ya nyingi ikiwa pamoja na tuzo ya muigizaji bora Afrika, Tuzo za Filamu na muziki za ...

RAIS SAMIA ASHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA MLEZI WA SKAUTI TANZANIA IKULU CHAMWINO DODOMA LEO HII

Picha
  Vijana wa Skauti wa Mkoa wa Simiyu Penina Mashimo kulia na Anastandhia Limbe kushoto, wakimvisha Skafu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipowasili katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo Oktoba 02, 2021 kwa ajili ya kuhudhuria katika Maadhimisho ya Siku ya Mlezi wa Skauti Tanzania. Kamishna Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Salum Hamduni akimkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mwongozo wa kuwawezesha na kuwafundisha vijana wa Skauti jinsi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Nchini, kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mlezi wa Skauti Tanzania yaliyoadhimishwa leo Oktoba 02, 2021 katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Mlezi wa Skauti Tanzania yaliyo...

WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA AZINDUA MSIKITI LEO HII KATIKA TARAFA YA IKWIRIRI WILAYANI RUFIJI

Picha
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa amefanya uzinduzi wa Msikiti Mkubwa leo ulipo katika Tarafa ya Ikwiriri wilayani Rufiji.  Mh. Majaliwa leo mapema amefikisha salamu za Mhe.Mbunge Wa Jimbo La Rufiji Mohammed Omar Mchengerwa Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Rais Menejimenti Ya Utumishi Wa Unma Na Utawala Bora pia amemuombea udhuru kutokana na majukumu aliyopewa na Mhe.Rais  ameshindwa kujumuika leo katika hafla hii ya ufunguzi wa Msikiti mjini Ikwiriri. Lakini pia Mhe.Waziri Mkuu hakuacha kuzungumzia suala la miundombinu wilayani hapo kwani amefikisha salaam kwa Wananchi juu ya ujenzi wa barabara ya Nyamwage-Utete yenye Km 37  kwa kiwango cha lami na kusisitiza kwamba mkataba wa ujenzi huu utasainiwa Jumatatu ijayo. Sambamba na hilo Mhe.Waziri Mkuu pia amewaeleza Wananchi wa Jimbo la Rufiji kuhusu ujenzi wa barabara ya Ikwiriri- Mkongo yenye Km 21 kwa kiwango cha lami. Pia Mhe.Waziri Mkuu amezungumzia ujenzi wa daraja la Mbambe litak...