Machapisho

AJALI MBAYA YATOKEA KARIAKOO USIKU HUU.

Picha
 Basi lililogonga treni likionekana kwa ndani mara baada ya ajali hiyo kutokea Taarifa iliyotufikia hivi punde, inaeleza kuwa Basi la UDA lenye namba za usajili T 696 CVP limegonga treni katika eneo la Kamata Jijini Dar es Salaam usiku huu wakati Basi hilo likotokea stendi ya Gerezani Kariakoo kuelekea Mbagala, inadaiwa kuna watu wamejeruhiwa katika ajali hiyo huku wengine wakidhaniwa kupoteza maisha. tutawaletea taarifa kamili baada ya kuipata kutoka vyombo vya Ulinzi wa Usalama jijini Dar es  salaam.  

MWANAMKE KUONGOZA MAREKANI?

Picha
Hilary Clinton amekuwa mwanamke wa kwanza kuongoza katika kinyang'anyiro cha urais ndani ya chama kikubwa nchini Marekani. Wajumbe wa Mkutano mkuu wa chama cha Democratic nchini Marekani wamemchagua seneta wa zamani na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje kuwa mgombea Urais kupitia chama hicho. Mpinzani wake mkuu Bernie Sanders alimaliza mchakato huo wa kuwania nafasi hiyo ya kukiwakilisha chama kwa kuwataka wajumbe, kumchagua Bi Clinton kwa kauli moja.

MAJALIWA: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII NI VEMA MKAJIPANGA VIZURI

Picha
waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kujipanga vizuri na kufanya mapitio ya idara zake hususan ya misitu baada ya kubainika kuwepo kwa matatizo makubwa. "Eneo la misitu limekuwa na matatizo makubwa, watendaji wengi si waaminifu na sura ya wizara si nzuri miti mingi inakatwa na fedha haiingii Serikalini. Huu ni mgogoro mpya" alisema. Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana alipokutana na watumishi wa wizara hiyo jana (Jumatatu, Julai 18, 2018) jijini Dar es Salaam, na kusisitiza kwamba hakuna sababu ya Serikali kuendelea kuwa na watumishi wasiokuwa na uaminifu, uadilifu na uwajibikaji Na: Yussuf Mufandish

SERIKALI YATOA BEI ELEKEZI YA SUKARI

Picha
  HATIMAYE  Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli  imekisikia kilio cha muda mrefu  cha Wananchi ambao  walikuwa wakilalamika kupanda  kwa  bei ya sukari nchini. Akizungumza na Waandishi wa Habari  mchana huu  jijini Dar es Salaam Mkurugenzi  mkuu wa Bodi ya Sukari nchini,Henry Semwaza amesema kuanzia sasa kilo moja ya  sukari itauzwa sh.  1800 nchi nzima. "Serikali, kupitia bodi ya Sukari Tanzania, inawaarifu wananchi wote kuwa bei ya rejareja ya sukari sasa itakuwa sh. 1,800 kwa kilo moja . "Amesema Semwaza na kuongeza; " Wafanyabiashara wote wanapaswa kuzingatia agizo hili, pamoja na kuhakikisha kuwa sukari inaendelea kusambazwa na kuuzwa kwa wananchi bila kuihodhi. "Maafisa biashara wa mikoa na wilaya watafuatilia na kusimamia utekelezaji wa agizo kuhusu bei elekezi ya sukari, na hawatasita kuchukua hatua stahiki za kisheria kwa wale watakaobainika kupandisha bei ya bidhaa hiyo. "

MAUAJI YA ALBINO NI AIBU KWA TANZANIA

Picha
Raisi wa Tanzania Jakaya Kikwete ameahidi kumaliza kabisa wimbi la mauaji ya Albino,na kusema kuwa waganga wa jadi wanahusishwa na mauaji hayo na kulitia aibu kubwa taifa lake lililoko Africa Mashariki. Wanaharakati wa haki za binaadamu wameeleza kuwa wimbi hilo limechukua uhai wa Albino sabini na tano nchini Tanzania tangu mwaka wa elfu mbili na viungo vyao kutumika katika masuala ya kishirikina. Raisi Jakaya Kikwete amesema kwamba hawezi kuruhusu hali hiyo iendelee kama ambavyo imekuwa ikitendeka kwa miaka iliyopita,haya ameyasema katika mazungumzo yake mapema wiki hii. Rais huyo anaamini katika ushirikiano kati ya serikali na wananchi, vita hii ya kuzuia mauaji ya watu wenye ualbino itafanikiwa kuepuka aibu hii kwa taifa la Tanzania. Inakadiriwa kuwa katika Tanzania nzima kuna Albino wapatao 200,000,na wengi wao hutambuliwa kutokana na rangi yao ya ngozi,macho na nywele zao . Waganga wa kienyeji huwaambia wateja wao kwamba viungo vya Albino huleta bahati ya kupendwa,mai...

AKATWA KICHWA NA KUPIKWA VIUNGO

Picha
SAMAHANI KWA PICHA HIZI MAANA ZINATISHA SANA, TUWIYANE RADHI Ni Tukio la kuskitisha sana ktk kijiji cha songambele wilayani MLELE mkoani KATAVI watu wasiofahamika wamemvamia mwenyekiti wa kijiji cha songambele na kisha kutenganisha kichwa na kiwiliwili na pia sehemu zake za siri na kisha kukata mkono wake mara mbili baada ya kufanya kitendo hicho walichukua viungo walivyokata kutoka kwa mwenyekiti huyo na kisha kuvitia kwenye sifuria wakaweka maji na kisha kubandika kwenye moto na kuanza kuvipika baada ya Tukio Hilo watu hao walitokomea sehemu isiyofahamika polisi wilayani MLELE wanaendelelea na uchunguzi kubaini wahusika wa tukio Hilo. Tukio Hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa saba ucku hayo ndo yaliyojiri wilayani kwetu MLELE.  

RAIS KIKWETE AAPISHA MAWAZIRI WAPYA IKULU

Picha
Tizama picha Moja wa Sura mpya katika baraza jipya la Mawaziri Naibu Waziri wa Elimu Anne Kilanngo Malecela akila kiapo Mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo,(PICHA NA FREDDY MARO) Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mawaziri na manaibu waziri aliowaapisha ikulu jijini Dar es Salaam jioni hii.Wanne kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue