Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2014

MCHAWI MTANZANIA AFUNGWA JELA MIAKA 3 KENYA

Picha
Vifaa walivyopatikana navyo washukiwa walipokamatwa na polisi Mchawi kutoka Tanzania amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu nchini Kenya kwa kumlaghai mwanamke mfanyabiashara mkenya na kumuibia shilingi milioni tisa. Mchawi huyo alimhadaa mama huyo kuwa kwa kupitia njia za kichawi angeweza kuzifanya pesa hizo kuwa maradufu yaani milioni 18. Bwana Amos Chipeta pia ataongezwa kifungo cha miezi tatu kwa kupatikana na vifaa vinavyoumiwa kufanya uchawi kama vile chupa, visu na ngozi ya Paka.  Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation, Chipeta alihukumiwa pamoja na mwenzake bwana Peter Christopher aliyepatikana na hirizi zinazotumika kufanyia uchawi. Bwana Chipeta alimlaghai Bi Catherine Njeri hela zake tarehe tofauti...

VICHWA VYA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MAY 29, 2014

Picha
                 

UN YASHUTUMU KUULIWA KWA MWANADADA WA KIPAKISTANI

Picha
Kamishna wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, aliyeshutumu mauaji ya mwanamke wa Pakistan. Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayesimamia Haki za Kibinadamu, Navi Pillay, amejiunga na maelfu ya watu duniani wanaoshutumu vikali mauaji ya mwanamke Mpakistani aliyepigwa mawe hadi kufa nje ya mahakama na wanachama wa familia yake kwa madai ya kuolewa na mwanamume aliyempenda. Mume wa mwanamke huyo - Mohammed Iqbal - ali sema kuwa alishtushwa na kukasirishwa na maafisa wa polisi waliokuwepo karibu na mahali palipotokea kitendo hicho lakini wakakosa kufanya lo lote kunusuru maisha yake. "Kilichotokea ni kibaya sana. Mmoja wa jamaa yangu alivua shati na kuwapungia maafisa wa polisi ili waweze kuingilia lakini wakapuuza. Walishuhudia kimyakimya tu Farzana akiuawa na wao hawakufanya lo lote," alisem...

IPO HAJA YA KUMSAIDIA BI MWANAIDI VUAI SALEH ALIYEUNGUA KWA MAJI YA MOTO

Picha
  Bi Mwanaid Vuai Saleh akiwa ameathirika kiasi hicho kama anavyoonekanav pichani akiwa katika hospitali ya Jeshi Bububu Unguja akiendelea na Matibabu yake akisubiri misaada ya Wasamaria wema ili kupata kusafirishwa nje ya nchi kupata matibabu zaidi ili kurudisha hali yake kiafya. Kwa  sasa amepata baraka zote kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar kupata missada kama inavyosomeka hapo chini.  Kumradhini kwa kuweka picha hii ya Bi Mwanaid Vuai Saleh, kwa maadili ya habari haifai. Aliyepata ajali hiyo ya  kuanguka wakati akiwa katika kazi zake za nyumbani na kuanguka katika sufuria la maji ya moto baada ya kuona kizunguzungu na kuangukia humo na kumuathiri kiasi hicho na kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Jeshi Bububu akipata matibabu ya majaraha hayo. Bi Mwanaid Vuai ni Mkazi wa Shehia ya Chumbini Wilaya ya Mjini Unguja  Anaomba msaada wa Fedha ili kusafirishwa nje ya Nchi kupelekwa India kwa matibabu  zaidi  Kwa...

SUAREZ AWATIMULIA VUMBI REAL MADRID, BARCELONA NA JEURI YAO YA PESA, ASEMA MAJOGOO NDIO HABARI YA MJINI

Picha
Mshambuliaji Luis Suarez amesema hana mpango wa kuondoka Liverpool licha ya kutakiwa na vigogo wa La Liga, Real Madrid na Barcelona MSHAMBULIAJI Luis Suarez amesema anapenda maisha ndani ya Liverpool na hafikirii kuondoka Anfield.Nyota huyo wa Uruguay amemaliza msimu vizuri akiwa na Wekundu hao wa Anfield kwa kufunga mabao 31 na kutwaa tuzo za Mwanasoka Bora wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA) na ya Waandishi wa Habari za Soka.Mafanikio hayo yanakuja baada ya kupitia msimu mgumu uliopita akifungiwa kwa kumng'ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic - akilazimisha kupita. Sasa wakati tetesi za usajili zimeanza tena, Suarez, ambaye mapema wiki hii alikanusha kuwa na nia ya kuhamia klabu nyingine kubwa Ulaya, ameamua kuuheshimu mkataba aliosaini Desemba mwaka jana. Furaha: Suarez alisaini mkataba mpya mapema msimu uliopita na amesema ana furaha kuwepo Liverpool Tuzo: Nyota huyo wa Uruguay alishinda tuzo ya mwaka ya PFA, huku Eden Hazard akishi...

NI MWAMKO MPAYA WA KISIASA NCHINI INDIA

Picha
Waziri mkuu mteule nchini India Narendra Modi Kuna mwamko mpya wa kisiasa nchini India ambapo chama cha kitaifa cha Hindu ,BJP kimeshinda uchaguzi uliokuwa na maamuzi makali kuwahi kufanyika nchini humo kwa kipindi cha miongo mitatu. Chama cha Congress ambacho kimelitawala taifa hilo kwa kipindi kirefu cha miaka 67 tangia uhuru wa taifa hilo kilishindwa vibaya. Huku kikiwa na idadi kubwa ya wabunge,chama cha BJP sasa kina uwezo wa kutawala taifa hilo bila ushirikiano na chama chochote. Wakati huohuo rais Barrack Obama wa Marekani amemkaribisha mjini Washington waziri mkuu mteule wa India Narendra Modi kufuatia ushindi mkubwa wa chama chake. Rais Obama alimpigia simu kiongozi huyo akisema kuwa anatarajia ushirikiano wa karibu mbali na kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili. ...

KATIBU MKUU WA CCM (KINANA) ASIMIKWA UCHIFU WA KABILA LA WANYAMWEZI

Picha
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu  Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa jimbo la Urambo,katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwananchi Skwea mjini Urambo,mkoani Tabora. Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnaye yuko katika ziara ya mikoa mitatu ya Tabora,Singida na Manyara,ya kuimarisha uhai wa chama,kukagua miradi mbalimbali ya maenedeleo inayotekelezwa na kusimamiwa na Serikali ya CCM,na pia kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyapatia ufumbuzi. Katika mkutano huo wa hadhara uliowakutanisha Wana Urambo kwa wingi,Kinana pia alisimikwa Uchifu wa kabila la Wanyamwezi.Kubwa zaidi Kinana pia alikabidhi piki piki 16 na baiskeli 95 kwa ajili ya watendaji wa chama cha CCM katika kata na matawi,zilizotolewa na Wabunge Mh,Samwel Sitta wa jimbo la Urambo Mashariki na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora,Mh.Magreth Sitta.  Baadhi ya Wananchi wa Mji wa Urambo wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Mwanan...

VICHWA VYA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI 17 MEI 2014

Picha
 

ANGALIA NA KUSIKILIZA DARSA ZA SHEIKH MUHAMMAD ALBIIDH

BOFYA HAPA

VICHWA VYA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI 15 MEI 2014

Picha
         

WANAJESHI WAMSHAMBULIA KAMANDA (NIGERIA)

Picha
Wanjeshi hao wamemlaumu kamanda wao kwa kusababisha mauaji ya wenzao Wanajeshi nchini Nigeria, wamemfyatulia risasi kamanda wao mkuu katika mji wa Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa nchi. Hata hivyo Meja Jenerali, Ahmed Mohammed alinusurika kifo. Shambulizi lilifanywa dhidi ya gari lake katika kambi ya jeshi ya Maimalari . Wanajeshi hao walimlaumu kamanda kwa mauaji ya wanajeshi wenzao walioshambuliwa na kundi la Boko Haram na kuuawa. Wakati huohuo, Rais wa Goodluck Jonathan amesema hayuko tayari kubadilishana wasichana miambili waliotekwa nyara na wapiganaji wa Boko Haram wanaozuiliwa katika magereza ya Nigeria.  Wazazi wa wasichana waliotekwa nyara na Boko Haram Waziri wa serikali awali alikuwa amesema kuwa maafisa wa utawala walikuwa tayari kwa mazungumzo na Boko Haram lakini Rais Goodluck Jonathan amesisitiza kwamba swala hilo halitazungumzi...

MWILI WA MTU WAKUTWA UKIELEA KWENYE MAJI YA MTO MKOKOZI (KONGOWE) DSM

Picha
Mwili wa mtu huyo ukielea kwenye maji ya Mto Mkokozi.   Mwili wa marehemu baada ya kutolewa nje kabla ya kuzikwa na jiji. Mwili wa mtu mmoja ambaye hakufahamika jina lake umeonekwa ukielea ndani ya Mto Mkokozi maeneo ya Kongowe jijini Dar es Salaam.....   Mwili wa mtu huyo ulipatikana baada ya wakazi wa eneo hilo kudai kuwa harufu kali ilikuwa ikitoka eneo hilo na ndipo waligundua maiti hiyo ambayo waliikuta ikiwa imeharibika kwa kiasi kikubwa. Sambamba na hilo pia zipo maiti nyingi ambazo zimeokotwa kutoka yombo kutokana na maafa ya mvua zilizonyesha wiki zilizopita nyuma.

MAADHIMISHO YA KITAIFA YA WIKI YA ELIMU TANZANIA YAFANYIKA DODOMA

Picha
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Ghalib Bilal akiwa na moja ya tuzo zilizotolewa kwa walimu wa Shule zilizofanya vizuri katika Elimu 2013 wakati wa kilele cha wiki ya Elimu, Kushoto ni Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Dkt Shukuru Kawambwa na Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi. Makamu wa Rais Dkt Ghalib Bilal akimpatia cheti Mwanafunzi Nelson Athon wa shule ya sekondari ya Kizilego iliyopo mkoani Bukoba baada ya kufanya vizuri mwaka jana.   MATUKIO YA PICHA  Mkuu wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Msalato ya Dodoma akiwa ameshika mfano wa hundi ya Milion 3 zilizotolewa na Selikari kama motisha kwa shule hiyo kupandisha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi kwa mwaka 2012/ 13 motisha hiyo imetolewa kwa jumla ya shule 14 za sekondari na 46 za msingi nchini, wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Elimu.  Mshairi wa  sanaa ya lugha katika Muziki Mrisho  Mpoto na Banana Zoro wakitoa B...